
Pangilia Herufi na Akili PC
Ubongo
Download Pangilia Herufi na Akili on PC With GameLoop Emulator
Pangilia Herufi na Akili on PC
Pangilia Herufi na Akili, coming from the developer Ubongo, is running on Android systerm in the past.
Now, You can play Pangilia Herufi na Akili on PC with GameLoop smoothly.
Download it in the GameLoop library or search results. No more eyeing the battery or frustrating calls at the wrong time any more.
Just enjoy Pangilia Herufi na Akili PC on the large screen for free!
Pangilia Herufi na Akili Introduction
Labda mtoto wako ameanza kujifunza alfabeti au ameanza kujifunza kupanga maneno, Pangilia herufi na Akili itamsaidia kuwa mpanga herufi mzuri mwenye kujiamini!
KWANINI UPAKUE PANGILIA HERUFI NA AKILI?
- NGAZI: Kila ngazi inayofuata ina changamoto zaidi kuliko iliyopita
- UBORA: imetengenezwa na timu ya watu waliobobea katika fani za elimu/ ufundishaji, uhandisi wa programu za simu ya mkononi, wabunifu wa michoro/ picha, watengenezaji wa katuni na uhandisi wa sauti
- UHAKIKISHO: Programu hii imebuniwa kulingana na matokeo ya utafiti ya jinsi watoto wadogo wanavyoweza kujifunza vizuri zaidi
- UTAMBULISHO: Akili ni mtoto mwenye miaka minne, mdadisi, mwerevu na anayependa kujifunza… mfano wa kuigwa kwa watoto wote
JINSI INAVYOFANYA KAZI
Chagua kati ya ngazi 16 kuanzia rahisi hadi ngumu! Kila ngazi inamkusanyiko wa maneno saba ya kupangilia, huku Ikiwa imepangiliwa kama mchezo na kuambatana na picha. Neno litatamkwa kwa sauti.
Kwenye ngazi rahisi, mpira wenye herufi utaondolewa kwenye neno na mchezaji atatakiwa kujaza herufi kwenye neno kwa kuweka mpira wenye herufi mahali sahihi. Kwenye ngazi ya juu, mipira tofauti tofauti yenye herufi imeondolewa hivyo mchezaji!
Kupangilia herufi, shika na usogeze mipira yenye herufi. Utakapokuwa unaisogeza utasikia matamshi ya herufi. Ukifanikiwa kuiweka mahali sahihi itabaki hapo, kama sivyo itarudi pale ulipoitoa.
FAIDA ZA KUJIFUNZA
* Jifunze na kuzoea kupangilia maneno kwa usahihi
* Jifunze uwezo wa kushirikisha mikono na macho
* Jifunze kutokata tamaa, jaribu mpaka ufanikiwe
* Cheza mwenyewe
* Furahia kucheza huku unajifunza
VIPENGELE MUHIMU
- Maneno 136 yaliyoambatana na picha
- Matamshi sahihi ya herufi na maneno
- Programu hii ni mahali salama kwa ajili ya mtoto wako kucheza
- Kwa ajili ya watoto wenye miaka mitatu, minne, mitano na sita
- HAKUNA maksi za juu, hivyo hakuna kushindwa wa la mkazo
- Inafanya kazi bila intaneti
JARIBU APP KATIKA KIINGEREZA
Kujifunza maneno yaliyo muhimu katika kiingereza, pamoja na jinsi ya kupangilia herufi zake, pakua App ya Spelling with Akili https://play.google.com/store/apps/details?id=com.enuma.ubongo.SpellingEN
KIPINDI CHA TELEVISION - AKILI AND ME
Akili and Me ni katuni zenye kuburudisha na kuelimisha kutoka Ubongo, watengenezaji wa Ubongo Kids na Akili and Me - vipindi vizuri vya kujifunza vilivyotengezwa Afrika kwa ajili ya Waafrika.
Akili ni mtoto mwenye miaka minne na mwenye udadisi, anaishi na famiia yake karibu na mlima Kilimanjaro, nchini Tanzania. Ana siri moja,kila usiku anapokuwa amelala, anaingia kwenye ulimwengu wa maajabu unaoitwa Lala land, ambako yeye na marafiki zake ambawo ni wanyama tofauti tofauti wanajifunza lugha, herufi, nambari na sanaa na wakati huohuo akijifunza ukarimu na kuanza kupatwa na hisia na mabadiliko ya haraka ya maisha ya mtoto mdogo!
Angalia video za Akili and Me kwenye mtandao au tembelea kwenye tovuti ya www.ubongo.org ili ujue kama vipindi vinaonyeshwa katika nchi yako.
KUHUSU UBONGO
Ubongo ni shirika la kijamii linalotengeneza vipindi vyenye kuelimisha na kuburudisha kwa ajili ya watoto barani afrika kwa kutumia teknolojia ambazo wanazo. Tunawaburudisha watoto waweze KUJIFUNZA na KUPENDA KUJIFUNZA!
Tunatumia nguvu ya burudani, vyombo vya habari, na simu za mkononi kuwafikishia vipindi vyenye ubora wa hali ya juu, kuelimisha, kuburudisha na vilivyotengenezwa kwa ajili ya mazingira yetu.
KUHUSU CURIOUS LEARNING
Curious learning ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kusambaza maudhui ya kujifunza kwa kila anaehitaji. Sisi ni timu ya watafiti, wasanidi programu na waelimishaji tuliojikita katika kuwapa watoto waliopo mahali popote na elimu ya kujua kusoma na kuandika katika lugha zao za asili kwa kutumia ushahidi na data.
KUHUSU PROGRAMU
Soma na Akili - Maeneo Mengi Tofauti! Imetengenezwa na mfumo wa Curious Reader uliotengenezwa na Curious Learning kwa ajili ya kutengeneza njia ya kusoma yenye kumhusisha mtumiaji.
Information
Developer
Ubongo
Latest Version
1.0.0
Last Updated
2019-10-07
Category
Educational
Available on
Google Play
Show More
How to play Pangilia Herufi na Akili with GameLoop on PC
1. Download GameLoop from the official website, then run the exe file to install GameLoop
2. Open GameLoop and search for “Pangilia Herufi na Akili” , find Pangilia Herufi na Akili in the search results and click “Install”
3. Enjoy playing Pangilia Herufi na Akili on GameLoop
Minimum requirements
OS
Windows 8.1 64-bit or Windows 10 64-bit
GPU
GTX 1050
CPU
i3-8300
Memory
8GB RAM
Storage
1GB available space
Recommended requirements
OS
Windows 8.1 64-bit or Windows 10 64-bit
GPU
GTX 1050
CPU
i3-9320
Memory
16GB RAM
Storage
1GB available space